![]() |
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI (Jeshi la Magereza)
TANZANIA
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, anatangaza nafasi za ajira kwa Vijana wa Kitanzania wenye elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) na wenye ujuzi katika fani mbalimbali kwa ngazi ya Stashahada na Shahada kama zilivyoainishwa katika Tangazo hili. Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
SIFA ZA MWOMBAJI:
a) Awe ni raia wa Tanzania.
b) Awe na Kitambulisho cha Uraia au Namba ya Utaifa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
c) Asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini.
d) Awe na umri kati ya miaka 18-24 kwa wahitimu wa Kidato cha Nne, na 18-28 kwa wenye ujuzi.
e) Awe na Cheti cha Kuzaliwa.
f) Awe na urefu usiopungua futi 5'4" kwa wanawake na futi 5'7" kwa wanaume.
g) Awe na siha na afya njema ya mwili na akili iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
h) Asiwe ameoa/kuolewa na asiwe amewahi kujifungua.
i) Asiwe na alama au michoro yoyote katika mwili wake (tattoo).
j) Awe na nidhamu na tabia njema na awe hajawahi kupatikana na hatia kwa shitaka la Jinai Mahakamani na hajawahi kufungwa.
k) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Askari Magereza na kufanya kazi mahali popote Tanzania Bara.
l) Awe tayari kujigharamia yeye binafsi katika hatua zote za awali za usaili wa ajira hii hadi kuripoti mafunzoni.
UJUZI NA FANI ZINAZOHITAJIKA:
a) Shahada ya Uhandisi wa Programu (Software Engineering).
b) Shahada ya Sayansi katika Teknolojia ya Vyombo vya Habari Mseto na Uhuishaji (Bachelor of Science in Multimedia Technology and Animation).
c) Shahada ya Usalama wa Mifumo (Bachelor of Cyber Security).
d) Shahada ya Uhandisi wa Mitandao (Bachelor in Network Engineering).
e) Shahada ya Saikolojia na Ushauri nasaha (Psychology and Councelling).
f) Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Uchimbaji Madini (Bachelor of Science in Mining Engineering).
g) Stashahada ya Ufundi wa vifaa vya Ofisi (Diploma in Office machine).
h) Stashahada ya Lugha za Alama (Diploma in Sign Language).
i) Stashahada ya Uuguzi (Diploma in Nursing).
j) Stashahada ya Mitambo ya Kilimo (Diploma in Agro-mechanization).
k) Stashahada ya Kilimo (Diploma in Agriculture).
l) Stashahada ya Mifugo (Diploma in Animal Health and Production).
m) Astashahada ya Katibu Muhtasi (Certificate in Secretarial).
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Ajira wa Magereza (Tanzania Prisons Service Recruitment Management System (TPSRMS)) ambao kiunganishi (link: https://ajira.magereza.go.tz) chake kimewekwa katika Tovuti ya Magereza. Maombi yatakayotumwa kwa njia nyingine hayatapokelewa.
ZINGATIA:
a) Waombaji wote ambao walishafukuzwa katika kozi za mafunzo ya awali ya uaskari magereza hawaruhusiwi kuomba tena.
b) Mwombaji yeyote atakayewasilisha nyaraka za uongo/kughushi (Forged Documents) au kuficha sifa halisi ya elimu atakuwa ametenda kosa la jinai hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 29 Agosti, 2025.
Imetolewa na: Jeremiah Y. Katungu, nac KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA.
15 Agosti, 2025.
BONYEZA /BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBO YAKO SASA HIVI