Nafasi za Kazi , Sihotech Engineering Company Limited - Wasimamizi wa Kazi (Foreman)

 SIHOTECH ENGINEERING COMPANY LIMITED

Nafasi za Kazi , Sihotech Engineering Company Limited -  Wasimamizi wa  Kazi (Foreman)
Nafasi za Kazi , Sihotech Engineering Company Limited -  Wasimamizi wa  Kazi (Foreman)



TANGAZO LA NAFASI ZA  KAZI



NAFASI: Wasimamizi wa  Kazi (Foreman)

MAHALI:  Dodoma na maeneo mbalimbali ya miradi  nchini Tanzania na Afrika  Mashariki

RIPOTI KWA:  Msimamizi wa Mradi  (Project Manager / Site Engineer)



Kampuni ya Sihotech  Engineering Co Ltd  inakaribisha maombi  kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu  na weledi kwa nafasi za Wasimamizi wa kazi (Foreman) katika kada zifuatazo:



1.1   MASONRY  FOREMAN- NAFASI 4
1.2  MAJUKUMU YA KAZI

• Kusimamia kazi za ujenzi wa kuta kwa matofali (blockwork)
•  Kusimamia kazi za upakaji wa plasta (plastering)
•  Kusimamia kazi za kumimina zege (concrete works)
•  Kuhakikisha vipimo na usahihi wa kazi kulingana na michoro ya mradi
•  Kusimamia mafundi  na kuwapa maelekezo ya kazi kila siku



2.1  STEEL FIXER FOREMAN-NAFASI 4
2.2 MAJUKUMU YA KAZI

•  Kusimamia ufungaji wa nondo kwenye kuta, nguzo, slab,  na boriti
• Kufuata vipimo sahihi vya michoro ya structural
• Kuandaa  orodha ya vifaa na mahitaji ya siku kwa mafundi



3.1 CARPENTER  (FORMWORK) FOREMAN-NAFASI  4
3.2 MAJUKUMU YA KAZI

•  Kusimamia kutengeneza  na kufunga formwork za slab, nguzo,  na boriti
•  Kusimamia mafundi seremala na kuhakikisha usalama  wa formwork kabla ya kumimina zege



4.1  PLUMBER  FOREMAN-NAFASI 4
4.2 MAJUKUMU YA KAZI

•  Kusimamia  usimikaji wa mifumo ya maji safi, maji taka na mvua
•  Kufanya vipimo na majaribio ya mabomba
•  Kusimamia mafundi  bomba na kuhakikisha ubora  wa kazi



5.1 WELDER FOREMAN-NAFASI 4
5.2 MAJUKUMU YA KAZI

•  Kusimamia kazi za kulehemu kwa matumizi ya miundo ya chuma
•  Kusimamia usalama  katika  matumizi ya vifaa vya welding


6.1   ELECTRICIAN  FOREMAN-NAFASI 4
6.2 MAJUKUMU YA KAZI

• Kusimamia usimikaji wa mfumo wa umeme (wiring, fittings, panels)
• Kufanya majaribio ya mfumo wa umeme kabla ya kuwasha
•  Kusimamia mafundi  umeme na kuhakikisha viwango vya usalama


7.1   PAINTER  FOREMAN-NAFASI 4
7.2 MAJUKUMU YA KAZI

• Kusimamia maandalizi na upakaji wa rangi  kwa majengo ya ndani  na nje
•  Kuhakikisha mchanganyiko sahihi wa rangi  na matumizi bora ya vifaa


8.1 TILE FOREMAN-NAFASI 4
8.2 MAJUKUMU YA KAZI

•  Kusimamia ufungaji wa vigae  (tiles) vya sakafu na ukutani
• Kusimamia ulinganifu wa vipimo na matumizi ya adhesive


SIFA ZA WAOMBAJI:
•  Uzoefu wa angalau  miaka 5 katika nafasi ya Foreman  kwenye miradi  ya ujenzi
• Uelewa mzuri  wa michoro ya ujenzi (construction drawings)
•  Uwezo wa kusimamia  mafundi na ratiba ya kazi
• Uaminifu,  uwezo wa kuwasiliana vizuri na kufuata maelekezo
• Vyeti vya kitaaluma (VETA/NACTE) ni kigezo cha ziada


JINSI YA KUTUMA  MAOMBI:
Maombi yote yaambatane na:
• Wasifu (CV)
•  Barua ya maombi
• Nakala ya vyeti husika
• Majina  na mawasiliano ya wadhamini watatu wa kazi


TUMA  MAOMBI  KWA:

WhatsApp: 0713 718 262/0766 612 285-  Meneja  Ujenzi
Barua pepe:  recruitment@sihotech.co.tz
Mwisho wa kupokea maombi:  1 Juni 2025

See: How to Send Your CV to an Employer the Right Way

See also: How to Prepare For a Panel Interview

For More up to date Opportunities Updates :

 Click / Tap Here to Follow the Fursa Opportunities channel on WhatsApp

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad