Nafasi za Kazi, Halmashauri ya Wilaya ya Songea - Ajira Mbalimbali

 

Nafasi za Kazi, Halmashauri ya Wilaya ya Songea - Ajira Mbalimbali
Nafasi za Kazi, Halmashauri ya Wilaya ya Songea - Ajira Mbalimbali

 Kumb. Na. HB.9/364/01/2                                                                              28/05/2025

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea amepokea kibali cha Ajira chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kutoka kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wote wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ifuatavyo: -

1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II - NAFASI 05

1.1 KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI


i.     Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri;
ii.    Kupokea wageni, kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
iii.     Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za
Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
iv.    Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
v.     Kupokea     majalada     na     kusambaza     kwa     Maofisa     walio      katika
Idara/Kitengo/Sehemu husika;
vi.     Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
vii.     Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
viii.     Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
ix.     Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa  Wahitimu  wa  Kidato  cha  Nne  (Form  Four)  wenye  Stashahada (Diploma)  ya  Uhazili  au  cheti  cha  NTA  level  6  ya  Uhazili.  Aidha,  wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 80 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.



1.1.2 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS C1 kwa Mwezi.
.


1.2    DEREVA DARAJA II - NAFASI 03

1.2.1   KAZI NA MAJUKUMU YA NAFASI ZA DEREVA


i.  Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari. ii.  Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
iii.  Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
iv.  Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
v.  Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari. vi.  Kufanya usafi wa gari.
vii.  Kufanya kazi nyingine kadri anavyoelekezwa na msimamizi wake.



1.2.2   SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV), au Sita (VI), awe na Leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving course) yanayotolewa na chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.2.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya mishahara mishahara ya Serikali – TGS B1.


MASHARTI YA JUMLA
i.    Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45
ii.    Waombaji    wote    waambatishe    maelezo    binafsi    yaliyojitosheleza    (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
iii.    Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao.
iv.    Maombi   yote   yaambatane   na   nakala   ya   vyeti   vya   Elimu   na   Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Diploma/Certificates, - Cheti cha mtihani  wa  Kidato  cha  IV  na  VI,  -  Computer  Certificate,  -  Vyeti  vya Kitaaluma.
v.    “Testmonial“, ‘‘Provisional Results “, “Statement of results “, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii.  Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
ix.    Waombaji  waliostaafishwa  katika  Utumishi  wa  Umma  hawaruhusiwi  kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
x.    Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi.     Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Juni, 2025.
xii.     Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ('Recruitment Portal').
xiii.    Maombi  yatakayowasiIishwa  nje  ya  utaratibu  ulioainishwa  katika  tangazo  hili hayata shughulikiwa.


Barua ziandikwe kwa Anwani ifuatayo; -

Ofisi ya MkurugenziMtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Songea,
1barabara ya Halmashauri, S. L. P 995,
57183 SONGEA, RUVUMA.


Imetolewa na; -



Elizabeth M. Gumbo
MKURUGENZI MTENDAJI (W)

Tuma Maombi Yako Kupitia Ajira Portal Hapa

 

Go to our Jobs page for more Similar Relevant Information. 

For More up to date Opportunities Updates :

 Tap / Click Here to Follow the Fursa Opportunities channel on WhatsApp


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad