![]() |
TAMISEMI: Tangazo la Kuitwa Kazini Nafasi za Kujitolea Katika Shule za Msingi kwa Kada ya Elimu Chini ya Mradi wa GPE - TSP. |
Tangazo la Kuitwa Kazini Nafasi za Kujitolea Katika Shule za Msingi kwa Kada ya Elimu Chini ya Mradi wa GPE - TSP.
Ofisi ya Rais-TAMISEMI inawatangazia waombaji wa nafasi za walimu wa kujitolea katika shule za msingi walioomba kati ya tarehe 17-30 Mei, 2025 kuwa majina ya waombaji waliokidhi vigezo yanapatikana kwenye tovuti ya www.tamisemi.go.tz.
Walimu waliokidhi vigezo wanatakiwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa walizoomba kuanzia tarehe 18 hadi 31 Agosti, 2025.
Wanatakiwa kwenda huko kwa ajili ya kujaza Mkataba wa Ajira ya Walimu wa Kujitolea na Mwajiri na pia kupatiwa barua za kupangwa vituo vya kazi.
Wanatakiwa kufika na Vyeti Halisi (Originals Certificates).
Walimu ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi.
Tangazo hili limetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI.
Anuani yao ni Mji wa Serikali - Mtumba, S.L.P. 1923, 41185 Dodoma.
Limetolewa tarehe 11 Agosti, 2025.
Orodha ya Walimu waliotwa kushika Nafasi za Kujitolea Katika Shule za Msingi kwa Kada ya Elimu Chini ya Mradi wa GPE - TSP.
BOFYA HAPA KUPAKUA ORODHA HII KAMILI KABISA
Madeni App: Mfumo Bora wa Kudai Madeni Uliotamadal na Kujitegemea (Automatiki)
For regular up to date Opportunities Updates :
Tap / Click Here to Follow the Fursa Opportunities channel on WhatsApp