Nafasi 17 za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Ya Temeke - Ajira Mbali mbali

 

Nafasi 12 za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Ya Temeke - Ajira Mbali mbali
Nafasi 12 za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Ya Temeke - Ajira Mbali mbali

Nafasi 17 za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Ya Temeke - Ajira Mbali mbali


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE

Kumb. Na. TMC/MD/M.13/112 VOL 1/45

Tarehe: 08/07/2025

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Manispaa ya Temeke kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/A/25 cha tarehe 29 April, 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II - NAFASI 05

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka /Majalada yanayohitajika na Watendaji (Action Officers)

ii. Kudhibiti upokeaji na uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka

iii. Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye rejista (Incoming Correspondence Register)

iv. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga nyaraka katika majalada

v. Kuorodhesha barua zinazotoka masijala kwenye rejista (Outgoing Correspondence Register)

vi. Kusimamia mfumo wa upelekaji wa barua, nyaraka na majalada kwa walengwa

vii. Kufanya “follow up” ya majalada/nyaraka zilizochukuliwa na watendaji na kuhakikisha zinarudishwa

viii. Kupokea, kupanga na kutunza kumbukumbu/nyaraka zote za ofisi

ix. Kupokea kumbukumbu/nyaraka kutoka Idara mbalimbali na kuziingiza katika mfumo wa kumbukumbu

x. Kupokea na kujibu hoja mbalimbali za kumbukumbu kutoka kwa wateja

xi. Kutambua majalada na nyaraka zisizotumika na kuzihifadhi mahala husika

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Awe amehitimu kidato cha Nne au Sita na Cheti cha Ufundi (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Pia awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

1.3 NGAZI YA MSHAHARA

TGS C


2.0 MWANDISHI MWENDELEZA OFISI DARAJA LA II - NAFASI 05

2.1 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kuandika barua na taarifa za kawaida na zile za siri

ii. Kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu wanazotaka kwenda

iii. Kuweka kumbukumbu na taarifa za matukio muhimu, miadi, tarehe za vikao na ratiba za kazi za Mkuu wake

iv. Kusaidia kutafuta na kurudisha majalada na nyaraka zinazohitajika

v. Kugawa majalada na nyaraka kwa maafisa na vitengo mbalimbali kwa maelekezo ya Mkuu wake

vi. Kuandaa na kusahihisha ajenda za vikao

vii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi

viii. Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Msimamizi wake

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Awe amehitimu kidato cha Nne au Sita mwenye Cheti cha Ufundi (Diploma) au NTA Level 6 katika masomo ya Ukatibu Muhtasi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe amefaulu Somo la Hatimkato Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika. Pia awe na ujuzi wa kutumia programu za kompyuta za Ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Email, Publisher).

2.3 NGAZI YA MSHAHARA

TGS C


3.0 DEREVA DARAJA LA II - NAFASI 07

3.1 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha usalama wa gari na abiria

ii. Kupeleka watumishi kwenye shughuli za kikazi

iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari

iv. Kutunza logbook ya gari

v. Kukusanya na kusambaza barua

vi. Kuhakikisha usafi wa gari wakati wote

vii. Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Msimamizi wake

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Awe amehitimu kidato cha Nne. Awe na leseni ya Udereva daraja la 'E' au 'C' yenye uzoefu wa kuendesha gari kwa angalau mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Pia awe na vyeti vya mafunzo ya udereva ikiwemo kozi ya msingi ya udereva (Basic Driving Course) kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

3.3 NGAZI YA MSHAHARA

TGS B


4.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.

ii. Waombaji wenye Ulemavu wanashauriwa kuomba na wanatakiwa kubainisha aina ya Ulemavu wao katika mfumo wa maombi.

iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa (Certified) na Wakili wa Serikali.

iv. Watumishi wa Umma waliopo kazini nafasi za ngazi ya kuingilia (entry level) hawataruhusiwa kuomba.

v. Kila mwombaji lazima aambatishe wasifu wake binafsi (Detailed CV) wenye anwani sahihi na namba za simu pamoja na majina matatu (3) ya wadhamini (Referees) wa kuaminika.

vi. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma (Academic Certificates) na Ufundi (Professional Certificates) vilivyothibitishwa (Certified True Copies) vikiwemo cheti cha Kumaliza Kidato cha Nne, Sita na Cheti kingine chochote kile cha Mafunzo kinachohusika na elimu ya mwombaji.

vii. ‘Testimonials', ‘Provisional results’, ‘Result slips’ (Matokeo ya muda ya Kidato cha IV na VI) HAVITAKUBALIWA.

viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).

ix. Waswataalam wa umma waliostaafu hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama ana kibali maalum kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi.

x. Waombaji ambao wanautofauti wa Herufi katika kitambulisho cha Taifa na Vyeti vya Taalum, Kidato cha Sita, Kidato cha Nne na cheti cha kuzaliwa wanatakiwa kuambatisha DEED POLL.

xi. Waombaji ambao wanautofauti wa Herufi katika kitambulisho cha Taifa na Vyeti vya Taalum, Kidato cha Sita, Kidato cha Nne na cheti cha kuzaliwa wanatakiwa kuambatisha AFFIRDAVIT (Kiapo).

xii. Waombaji wa kazi ya Dereva Daraja II wenye Leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo vya udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.

xiii. Waombaji watakao wasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

xiv. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 22/07/2025

MUHIMU: Kumbuka Kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, Anuani ya barua hiyo ielekezwa kwa;

MKURUGENZI WA MANISPAA,

HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE,

S. L. P 46343,

DAR ES SALAM.

xv. Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira Serikalini (Recruitment Portal) kupitia anwani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz.

xvi. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliotajwa hapo juu HAYATASHUGHULIKIWA.

Go to our Jobs page for more Similar Relevant Information. 

See also: How to Send Your CV to an Employer the Right Way

Check out : How to Use the Government’s Official Ajira Portal

See also:   Ufugaji wa Kuku: Njia Bora na Yenye Faida Kubwa ya Kujiajiri

 

For More up to date Opportunities Updates :

 Tap / Click Here to Follow the Fursa Opportunities channel on WhatsApp

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad