Nafasi 11 za Kazi kutoka Halmashauri Ya Manispaa Ya Kinondoni - Dereva Daraja La II

 

Nafasi 11 za Kazi kutoka Halmashauri Ya Manispaa Ya Kinondoni - Dereva Daraja La II

 Nafasi 11 za Kazi kutoka Halmashauri Ya Manispaa Ya Kinondoni - Dereva Daraja La II

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

Unapojibu tafadhali jibu: Kumb. Na. CHB.148/505/01/35

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

04 Julai, 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali cha Ajira mpya chenye Kumb.Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29.04.2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1.0 DEREVA DARAJA LA II - NAFASI 11

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.

  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.

  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.

  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.

  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.

  • Kufanya usafi wa gari.

  • Kufanya kazi nyingine kadri anavyoelekezwa na Msimamizi wake.

1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe amehitimu Kidato cha NNE (Form IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne (IV).

  • Awe na Leseni ya Daraja la 'E' au 'C' ya uendeshaji magari pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika na awe amehudhuria mafunzo ya Msingi ya uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA

  • Kwa kuzingatia Ngazi ya mishahara ya serikali- TGS B.


Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45.

  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.

  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E mail Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate - Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne na cha Sita, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).

  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USA1ILI.

  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).

  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

  • Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.

  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. САС. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.

  • Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.

  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Julai, 2025.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:

MKURUGENZI WA MANISPAA,

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI,

S.L.P 31902,

DAR ES SALAAM

  • Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielekroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/advert/display_advert/11078 

    Recruitment Portal (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment Portal').

  • Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulio ainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tangazo hili limetolewa na;

Hanifa S. Hamza

MKURUGENZI WA MANISPAA

Nafasi 11 za Kazi kutoka Halmashauri Ya Manispaa Ya Kinondoni - Dereva Daraja La II 


Mawasiliano

Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni, S.L.P. 31902, 2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad